Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Donald Trump” Rais mteule wa Marekani amesema kwamba serikali yake itatilia mkazo suala la kupambana na Daesh nchini Syria na si kumuondosha Rais wa nchi hiyo katika utawala wake.
Rais mteule wa Marekani aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Wall Street na kusisitiza kuwa: kuisaidia serikali ya Syria katika kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh ni katika mambo ya msingi yanayotakiwa kusimamiwa na serikali ya Marekani.
Aidha amesisitiza akibainisha kuwa kuisaidia serikali ya Asad ndio njia pekee ya kuwasambaratisha magaidi, ambao wanaifanya nchi hiyo kuwa katika machafuko.
Rais mteule wa Marekani amesema: mtazamo wangu unatafautiana na mitazamo ya wengi, mimi naona kuwa mupo katika vita nchini Syria, hali yakuwa majeshi ya Syria yanapambana dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh hivyo ni vyema kushikamana na Syria katika kuvisambaratisha vikundi vya kigaidi ikiwemo kikundi cha Daesh.
Aliongeza kusema kuwa serikali ya Urusi kwa sasa imeshikamana na kujiunga kikamilifu na serikali ya Syria, kwa upande mwingi Iran ambayo inaelekea kuwa katika nchi ziliokuwa na nguvu Dunia pia imeungana na Syria katika kuvisambaratisha vikundi hivyo...(jambo la kushangaza) sisi tunavisaidia vikundi vya kigaidi katika kukabilia na serikali ya Syria, bila ya kufahamu kuwa vikundi hivyo ni vya vinatoka wapi!?
Donald Truampo amesema: endapo sisi tukaingia vitani kwaajili ya kumtoa Rais wa Syria madarakani maana yake tunaanza vita na serikali ya Urusi.
Rais mteule wa Marekani aliendelea kusema kuwa: hivi punde nimepokea barua yenye maneno mazuri kutoka kwa Rais wa Urusi, ambapo haraka iwezekanavyo nitaongea naye kwa simu.
Rais wa jamhuri ya Marekani pia amezungumzia suala Palestina na Israel, huku akitoa matumaini kuwa pande hizo mbili zitafikia muafaka kupitia yeye, hii ni katika hali ambayo Trump mara nyingi alikuwa akisema kuwa sula la Palestina na Israel ni suala la kivita ambapo kamwe halitaweza kumalizwa.
mwisho wa Habari/290